NA MWANDISHI WETU, WASHINGTON DC
MWENYEKITI, Katibu na Mweka hazina, wa Jumuia ya Watanzania waishio Marekani, wanashutumiwa na wanajumuia wa Washignton kuwa wamepokea rushwa kutoka kwa Chadema kwa ajili ya kufanyia pickic na party ya usiku, vitakavyofanyika Jumamosi hii, Agosti 25, 2012.
Habari za madai za shutuma hizo zinasema kuwa Jumuia ilikuwa na fedha taslim zisizozidi Dola 2000 za Marekani zinazotosha kufanya party ya mchana ya picnic peke yake, lakini kwa cha kushangaza wakati wanajumuia wakiwa wanahoji kwa nini party ya usiku ifanyike wakati Jumuia haina fedha za kutosha, Viongozi hao wameweza kuja na fungu kubwa la fedha ambazo watazitumia kufanya party zote mbili kubwa na za kifahari zitakazoambatana na chakula na vinywaji mchana na usiku bure.
Kama haitoshi kutokana na fungu hilo, pombe zitakuwa za bure hadi saa nane usiku, wakati ukumbi na muziki vikiwa vimelipiwa kwa Cash siyo mkopo.
“Habari za kuaminika na ushahidi upo zinasema kuwa Katibu wa Jumuia Bwana Amosi Cherehani ni Mweka hazina wa Chadema Washigton na ndiye ambaye ameweza kuhamasisha fedha hizo kutoka Chadema iliziweze kufanya hafla hiyo”, Imsema taarifa iliyotumwa kwa mtandao kutoka Marekani.
“Wananchi wanahoji kwa nini Mwenyekiti ambaye alichaguliwa kwa kishindo ameweza kukubali kadia hii wkati Jumuia haifungamani na chama chochote cha siasa?” Imehojiwa katika taarifa hiyo.
“Kutokana na kadhia hiyo, wakereketwa wa Jumuia wameipa Mamlaka Kampuni ya ERNEST & YOUNG kufanya ”INDEPENDENCE AUDITING” ya Jumuia ili kujua “INCOME AND EXPENDITURE za Jumuia yao zometoka wapi na zimetumika vipi kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa”, Taarifa imesema.
Tarrifa imesema wanajumuia wanaomba kuitisha mkutano ili kupiga kura a maoni ya kutokuwa na imani na uongozi kwakuwa bado mchanga. ..”Na tuliuchagua kwa imani, hatutaki vyama vya siasa vituingile…Rushwa ni adui wa Haki”
Copyrights Tabitha Hudson 2012
0 comments:
Post a Comment