Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi Agosti, 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kukamilisha zoezi la kujibu maswali husika katika zoezi hilo, leo asubuhi nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe.
===== ====== ======
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASHIRIKI ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.
Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Box 5380 Dar es Salaam.
Copyrights Tabitha Hudson 2012
0 comments:
Post a Comment