KWA sasa mambo yanazidi kunoga wakati sikukuu ya Idd El Fitr ikiwa inakaribia, pale kulipoandaliwa burudani ya kufa mtu katika fukwe ya Coco iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam siku ya Idd Pili.
Katika burudani hiyo inayoletwa na vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi, huku wasanii kadhaa wenye majina wakitarajiwa kufanya kweli zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, wameamua kuleta burudani hiyo ambayo itakuwa bure kwa kila atakayeshiriki, huku kukiwa na michezo kibao ya kuvutia.
Consolata alisema, wasanii watakaoshiriki katika burudani hiyo ya kufa mtu siku hiyo ni pamoja na Roma Mkatoliki pamoja na kundi za la TMK Wanaume.
Kundi hilo linajulikana kwa jinsi lilivyo na wasanii wakali kama Mheshimiwa Temba, Chege, Aslay, Bibi Cheka na wakali wengine kibao, ambao wote wameapa kutoa burudani ya kufa mtu.
“Unajua vinywaji hivi havina kilevi, hivyo ni vema mtu ukaja na familia yako kwani kutakuwa na michezo ya kila aina pamoja na zawadi kibao,” alisema.
Consolata alisema, burudani hizo za bure zitaanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni katika siku hiyo ya Idd Pili.
Copyrights Tabitha Hudson 2012
0 comments:
Post a Comment