Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. NA MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kwamba mtu yoyote ambaye anona hakutendewa haki kuhusu kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi anaweza kutafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani. Kauli hiyo ameitoa leo Bungeni wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni , Freeman Mbowe, lililouliza kuwa Julai 30, mwaka huu, Serikali ililifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Maadam katika siku za hivi karibuni serikali imetambua umuhimu wa mahakama ni kwanini wamelifungia gazeti hili badala ya kulipeleka mahakamani na wahusika wapate nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa? Akijibu swali hilo , Waziri Mkuu Pinda, alisema ni kweli serikali imechukua hatua hiyo, lakini imechukua hatua hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi na “mtu yoyote kwa msingi wa sheria hiyo kama anaona hajatendewa haki basi ni juu yake kutafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani,” alisema Waziri Mkuu Pinda. Katika swali lake la nyongeza la kiongozi huyo lililouliza kuwa Sheria iliyotumika imekuwa ikilalamikiwa na wadau wengi na vyombo vya habari kwa muda mrefu . Je wewe huamini kwa kutumia sheria hiyo ni kinyume haki na ni msisitizo wa utawala usio bora? Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Pinda alisema “ Mimi siamini hivyo kwa sababu sheria hiyo imetungwa na Bunge tukufu na kuwa bado inatumika na ni sheria halali, sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapobadilishwa''. alisema Pinda. |
Copyrights Tabitha Hudson 2012
0 comments:
Post a Comment