Obama's slumdog brother: Kutana na mlevi asiye na matumaini aishie jijini Nairobi ambaye ni mdogo wake na rais wa Marekani
Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye gazeti la Daily Mail mwandishi akiwa ANDREW MALONE. Makala hii imechapishwa jana, August 10, 2012.
Wakati mwanaume mrefu na anayejulikana sana akiondoka kwenye kibanda chake kilichopo kwenye makazi fukara kabisa barani Afrika wiki hii, baadhi ya watu walianza kumuita kwa utani:‘Mister President! Mister President!’
Akielekea kupata kifungua kinywa huku akivuka mifereji inayotiririsha maji machafu, muonekano wa jamaa huyu mrefu na aliyekonda, unavutia vicheko vya chini chini kutoka kwa watoto wanaocheza kwenye jalala.
George akiwa kwenye nyumba anayoishi |
Jina la jamaa huyu ni George Hussein Obama, ni mdogo wake na Barack Hussein Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani na mwanaume anayeheshimika zaidi duniani.
Wanaume hawa wawili wanachangia baba lakini Barack Obama alizaliwa Hawaii kwa mke wa pili wa baba yao ambaye ni mmarekani na George alizaliwa nchini Kenya akiwa mtoto wa mke wanne wa mzee huyo.
Leo, wakati Barack akifurahia maisha kwenye Ikulu ya White House, akiruka kwenda nje na Air Force One na ni rafiki wa mastaa wa filamu na wengine mashuhuri, George, 30, anapatikana akiwa amechoka kwenye makazi yake ambayo hata wakazi wenzake wa eneo hilo maskini jijini Nairobi wanayaona kama kichuguu.
Ingawa anadai kutotumia heroin au cocaine, George hutumia muda mwingi kunywa Gongo (Chang’aa) kuanzia anapoamka mpaka muda ambao huanguka na kuzima kabisa.
Gongo anayokunywa ni ile iliyochanganywa na kemikali ya ethanol, na kuongezea acid kutoka kwenye betri ili kuipa kick zaidi, na mchanganyiko huu husababisha upofu na kifo inapochanganywa vibaya.
Kiasi kidogo tu cha pombe hiyo huwafanya hata wanywaji wazoefu kulewa kiasi cha kushindwa hata kukumbuka majina yao. Wanywaji wa mara kwa mara huathrika maini na figo ama ubongo.
Nilipomtafuta George asubuhi siku moja kufahamu maisha yake, alikuwa tayari kwenye kibanda kimoja jirani akinywa Chang’aa ambapo ngono na machangudoa ni sehemu ya menu na hufanyika kwenye kitanda kilichowekwa nyuma.
Utambulisho unafanywa na ‘mpambe’ wa George — mkazi wa eneo hilo mwenye macho mekundu na mnywaji mwenzie ambaye anamvuta George nje ya kibanda hicho na kumwabia aje kumuona mzungu nje (shouting at him to come and see the ‘muzungu’ (white man) outside.
Baadaye baada ya kusalimia, ninafanya kosa. Namkaribisha George kwaajili ya chakula cha mchana kwenye hoteli yangu. Kwa siku mbili zilizofuatia, aliivamia baa yangu ndogo, kuwaalika wapenzi wake kibao na washkaji zake kula na kunywa kwa gharama zangu na kujionesha kama staa aliyeharibikiwa.
Aliomba pia ‘kitu kidogo’ — Swahili for something small, which, of course, means something large and financial — na alichukia baada ya mimi kukataa kuwapa hela mademu zake.
George pia aliendelea kulaumu kuhusu jina la Obama kuwa kama mzigo na laana kwake, ilhali wakati mwingine bila aibu hulitumia jina hilo kupata hela nyingi iwezekanavyo ili kuzitumia kunywa na kuvuta bangi.
‘Watu wanavutiwa na mimi kwasababu ya kaka yangu,’ anashusha pumzi na kushusha Johnnie Walker mbili kwa mpigo. ‘Nachukia’. Watu wanapenda niwe mtu mwingine.’
Mara ya kwanza George alikutana na kaka yake alipokuwa shule ya msingi. Barack alienda Nairobi miake michache tu baada ya baba yao kufariki kwa ajali ya gari. George anakumbuka alikuwa akicheza soka wakati kaka yake alipowasili kumsalimia.
Mara ya pili wanakutana ni kipindi Obama — alipokuwa Senator na alifanya ziara ya Afrika Mashariki mwaka 2006, na kutembelea Nairobi kuiona familia yake.
George anasema kwa sasa watu wanamshinikiza afuate nyayo za kaka yake kwenye siasa. ‘Nina watu wengi ambao huniambia nigombee ubunge. Lakini sivutiwi na siasa.’
Kisha anatulia, na kuongeza: ‘Lakini kama Barack angekuwa rais na mimi ningekuwa rais wa Kenya ingekuwa rahisi kuonana.’
Anasema umaskini wake ndio unawazuia ndugu hao kuwa na uhusiano wa karibu.
‘Ana majukumu. Hatakiwi kunilea mimi,’ anasema. Mimi ni mtu mzima, kila mtu hudhani kuwa huwa ananitumia fedha. Lakini mimi sio ombaomba.’ Lakini alipoulizwa iwapo aatachukua fedha akipewa na Obama alisema: ‘Seriously! Yes! Who wouldn’t?’
George alikulia jijini Nairobi akiwa na mama yake ambaye aliolewa tena na mfaransa aliyekuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada jambo ambalo anadai lilimfanya awe hivyo.
Alianza kunywa pombe na kuvuta bangi akiwa na miaka kumi, miaka mitano baadaye alifukuzwa kwenye shule ya boarding, ambako alicheza rugby na kujifunza lugha za kigeni kutokana na kutumia madawa ya kulevya.
Anakubali kuwa alikuja kuwa addicted na cocaine na heroin akiwa na miaka 17, na kuwa mwizi wa kutumia silaha ili kupata hela ya kunywea pombe.
Mwaka 2003 alifungwa jela kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha.
Alikaa kwa miezi tisa kabla ya kutoka kutokana na kukosekana ushahidi.
Swali ni je! George anastahili kuishi maisha haya wakati kaka yake ni rais wa Marekani?
0 comments:
Post a Comment