Ads 468x60px

Thursday, July 11, 2013

CHISSANO NA MBEKI KUFUATILIA MGOGORO WA ZIWA NYASA

Chissano, Mbeki, kufuatilia mgogoro wa Ziwa Nyasa Marais wa zamani wa Msumbiji na Afrika Kusini wanatarajiwa kuelekea nchini Malawi siku ya Jumapili ili kuzungumza na viongozi wa nchi hiyo kuhusu mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Malawi na Tanzania.

Joachim Chissano na Thabo Mbeki watafanya mazungumzo na Rais Joyce Banda, Waziri wa Mambo ya Nje na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Malawi kabla ya kuelekea Tanzania kwa mazungumzo kama hayo. Tanzania na Malawi zimekuwa zikivutana kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa ambapo Malawi inadai mpaka wake na Tanzania upo katika ufukwe huku Tanzania ikidai kwamba mpaka uko katikati ya ziwa. Hii ni Mara ya kwanza kwa Chissano na Mbeki kufuatilia rasmi kadhia hiyo tangu iwasilishwe kwenye jukwaa la marais wastaafu wa Jumuiya ya SADC mwaka huu.

0 comments: