Ads 468x60px

Thursday, August 30, 2012

MALINZI AVUNJA UKIMYA AKIZINDUA ROCK CITY MARATHON 2012

 Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Dioniz Malinzi akiongea na waandishi
wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio za nne za Rock City Marathon
2012 zitakazofanyika Oktoba 28 jijini Mwanza
 Picha
tofauti za wawakilishi wa Makampuni na Mashirika yanayodhamini mbio za
Rock City Marathon 2012, wakizungumza mbele ya waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa mbio hizo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar
es Salaam leo mchana
 Wawakilishi
wa Makampuni na Mashirika yanayodhamini mashindano ya mbio za Rock City
Marathon 2012, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mbio
hizo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam leo


 Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania, Tullo Chambo (wa pili kushoto),
akifuatilia uzinduzi wa Rock City Marathon 2012 akiwa pamoja na Mweka
Hazina wa RT, Suleiman Is Haq (mwenye shati jeupe) kwenye hoteli ya New
Africa jijini Dar es Salaam leo.


DAR ES SALAAM, Tanzania


JITIHADA za wazi baina ya serikali kupitia
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Baraza la Michezo la
Taifa (BMT), vyama vya michezo, mashirika na wadau wengine zinahitajika,
ili kurejesha heshima iliyopotea miongoni mwa michezo na wanamichezo wa
Tanzania, hususani riadha.


Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo na
Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio
za Rock City Marathon 2012 uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa. 


Malinzi alisema kuwa, kama Mwenyekiti wa
BMT, anatambua kudorora kwa michezo hasa riadha nchini, hali iliyotokana
na vyama kujaza ‘wachumia tumbo’ katika nyadhifa zake, jambo
linalochangia ukosefu wa changamoto mpya za maendeleo.


“Michezo imedorora na kimsingi inatia aibu.
Taifa kama hili lenye watu zaidi ya milioni 40 kuwakilishwa na watu
sita katika Olimpiki 2012. Wanachofanya wenye dhamana kwenye vyama ni
ufisadi, unaopaswa kukomeshwa sasa, ikiwa tunataka kupata maendeleo ya
michezo,” alisema Malinzi.


Aliongeza kuwa, BMT imefurahishwa na
mafanikio waliyopata waandaaji wa Rock City Marathon, kampuni ya Capital
Plus katika kuendesha mbio hizo kwa mwaka wa nne na kuwa, baraza lake
liko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kwa kampuni hiyo na nyingine
kufanikisha matukio yenye nia ya kulipa heshima taifa kupitia michezo.


Alisisitiza kuwa, aibu ya kuvurunda
Olimpiki 2012 ni ya kujitakia, kutokana na kuona ufisadi bila kuchukua
hatua katika vyama vya michezo, huku viongozi wake wakiwekeza katika
kujijengea majumba ya kifahari na kuacha michezo husika ikikosa dira.
Malinzi,
alienda mbali zaidi na kuzungumzia hatua ilizochukua BMT, baada ya
kubaini ubabaishaji mkubwa katika Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
ambako viongozi waliokuwepo walikuwa wakipitisha muda wao wa kukaa
madarakani makusudi, ambako walifanikiwa kufanikisha kufanyika kwa
uchaguzi kwa mbinde ambao umeleta changamoto mpya.


Aligeukia mashirika na vyama vya michezo,
vinavyokumbatia mashindano na matukio yasiyo na tija kwa michezo na
wanamichezo na kutaka vita dhidi ya taasisi za aina hiyo kuwa kali, ili
kurejesha heshima ya riadha, mchezo uliyoipa Tanzania sifa kubwa nje ya
mipaka.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Capital
Plus, Dk. Ellen Otaru Okoedion, alisema kuwa, Rock City Marathon (RCM),
inatarajiwa kufanyika Oktoba 28 jijini Mwanza na kuwa, kampuni yake
inajivunia mafanikio yaliyopatikana kwa miaka minne.


Alisema RCM 2012 itakuwa chini ya
kaulimbiu; ‘Utalii Kupitia Michezo’, sera itakayosaidia kutangaza
vivutio mbalimbali vya utalii.


Mbio hizo zinadhaminiwa na PPF, NSSF, TTB,
TANAPA, Geita Gold Mine, African Barrick Gold, Air Tanzania, Sahara
Communications, Nyanza Bottlers, Airtel Tanzania, New Mwanza Hotel, New
Africa Hotel na zitashirikisha wanariadha wa rika tofauti kuanzia watoto
hadi watu wazima.

0 comments: