Ads 468x60px

Sunday, August 12, 2012

RAIS KIKWETE AONANA NA RAIS MPYA WA GHANA, ATEMBELEA MASHAMBA YA MANANASI




Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana
nyumbani kwake jijini  Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya  kumtembelea
na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John
Evans Atta Mills aliyezikwa jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani
kwake jijini  Accra leo Agosti 11, 2012  wakati alipomtembelea
kiongozi huyo mpya wa Ghana na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais
wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya
kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms
Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti
11, 2012
 Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi
yanayolimwa  kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la   Bomarts
Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam  nje kidogo ya
jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa
shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa
Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya  mananasi katika
shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra.
Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B.
Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27.
Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya
1980 kujionea ukulima huo wa matunda.


Copyrights Tabitha Hudson 2012

0 comments: