Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, Bi. Fatou Bensouda, ameondoa mashahidi watatu kwenye kesi ya jinai dhidi ya binadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Bensouda amesema mashahidi wawili wamesema kwamba hawawezi kuendelea kuwa mashahidi kwenye kesi hiyo kutokana na kuhofia usalama wao,pi ametathmini ushahidi wa shahidi mwingine na ameona hauna umuhimu mkubwa na kuamua kumuondoa.
Mahakama ya ICC majuma kadhaa yaliyopita iliamua kwamba, Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto atahudhuria vikao muhimu tu vya kesi yake mjini Hague na kisha kushiriki vikao vya kawaida kwa njia ya video.
Wachambuzi wa masuala ya kisheria wanasema hatua hiyo ina maanisha kwamba kesi dhidi ya Rais Kenyatta na Makamu wake zinaendelea kuwa dhaifu na huenda wakafutiwa mashtaka iwapo matukio kama hayo yataendelea kushuhudiwa.
0 comments:
Post a Comment