Mahakama moja ya Nigeria imewahukumu kifungo cha maisha jela
wanachama wanne wa kundi la Boko Haram kwa kuhusika katika mashambulizi
matatu makubwa ambapo walitumia mada za miripuko za viwandani karibu na
Abuja mwaka 2011.
Mbali na hao wanne, mwanachama mwingine wa tano wa Boko Haram
amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela na wa sita ameachiwa huru kwa
kukosekana ushahidi.
Kundi la Boko Haram linadai kuwa mfumo wa Magharibi wa elimu ni
haramu na linafanya mashambulizi yake dhidi ya kila mtu anayepinga fikra
hiyo.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, hadi kufikia sasa
zaidi ya watu elfu tatu wameuliwa na na kundi la Boko Haram huko
Nigeria, mashambulizi ya karibuni kabisa yakiwa ni yale yaliyofanywa na
kundi hilo kwenye shule moja ya jimbo la Yobe la kaskazini mwa Nigeria
na kupelekea kuuawa wanafunzi 41 na mwalimu mmoja.
Gavana wa jimbo hilo la la Yobe la kaskazini mwa Nigeria ametoa amri
ya kufungwa shule zote za sekondari katika jimbo hilo hadi mwezi
Septemba, ili kuepusha mashambulio zaidi ya kundi la Boko Haram kwenye
shule za jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment