Ads 468x60px

Wednesday, August 08, 2012

Taswira:Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na Familia Yake Wapata Ajali


 Gari la Naibu waziri wa
Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah likiwe limepinduka
Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah
--
 Mzimu wa ajali kwa wabunge na viongozi
wa Taifa umeendelea kushika kasi hapa nchini baada Naibu waziri wa
Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata
ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali
hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo
akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na
watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa
hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video
amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori
alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .

Imeelezwa
baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo
hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya
raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .

Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na
kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye
ameumia kichwani."

Taarifa
ambayo nimeipata kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni na
tayari nimewasiliana na kamanda wa polisi wa mkoa huo na amekwenda eneo
la tukuio"alimueleza mdau Francis Godwin kwa njia ya simu

0 comments: