Ads 468x60px

Friday, October 19, 2012

TIGO YAANDAA ONYESHO LA SARAKASI KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO (SME).



Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Mama Afrika  wakionyesha umahiri wao wakati wa onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika lililoandaliwa na Tigo kwa wafanyabiashara wadogo jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kikundi cha sarakasi  Mama Afrika  wakionyesha umahiri wao wakati wa onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha cha Mama Afrika wakionyesha umahiri wao wakati wa onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika Circus lilidhaminiwa na Tigo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliohudhuria onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika lililodhaminiwa na Tigo wakishanglia huku wakiwa hawaamini macho yao kutokana na umahiri uliokuwa ukionyeshwa na wasanii kwa kundi la sarakasi la Mama Afrika jinni Dar es Salaam.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imesema itaendelea kudhamini sanaa mbalimbali nchini ili kuleta burudani kwa watanzania na kukuza wigo wa ajira nchini.
Akizungumza katika onyesho maalumu la sarakasi la Tigo Mama Afrika waliloliandaa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo jijini Dar es Salaam juzi, Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa  Tigo, Gaudensi Mushi alisema, kampuni yao itaendelea kudhamini sanaa za maigizo kwani zinasaidia sana katika kuongeza soko la ajira nchini.
Bwana Mushi alisema mbali ya kuwa maonyesho ya sarakasi ya Tigo Mama Afrika yamekuwa kivutio kikubwa kwa kila mtu anayefika katika ukumbi huo wa New World Cinema lakini pia yamekuwa na faida kubwa kwa wasanii wanaounda kundi hilo ambao asilimia kubwa ni watanzania.
“Tigo inafuraha kubwa kuendelea kusapoti sanaa kama hizi kwani zinaburudisha na pia zinaweza kuwakomboa wasanii wenyewe kiuchumi,” akasema Mushi.
Mmoja wa wafanyabiashara walioalikwa katika onyesha hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Viviani Charles kutoka kampuni ya La Petite ya jijini humo aliipongeza Tigo na kusema kuwa maonyesho hayo ni mazuri sana na kuwataka vijana wakitanzania kuachana na dhana ya kuwa hakuna ajira bali kuiga mfano ya kikundi hicho cha sarakasi.
Mfanyabiashara  mwingine aliyejitaja kwa jina la Mustafa Sulemanjee mbalina kuisukuru kampuni hiyo ya simu za mkononi alionyesha mshangao wake kwa jinsi vijana hao wa kitanzania walivyoweza kuonyesha umahiri wao katika sanaa hiyo ya sarakasi. 
Hii ni mara ya nane kwa Tigo kudhamini makundi mbalimbali kwenda kushuhudia maonyesho hayo ya sarakasi yanayoendelea katika ukumbi huo mara baada ya hivi karibuni kudhamini onyesho maalumu kwa ajili ya  wanafunzi wa shule ya tatu za sekondari, na pia kwa ajili ya watoto yatima. 

Copyrights Tabitha Hudson 2012

0 comments: