Nyota Tumaini Letu ni mpango wa Image Profession kwenye program yake ya id's-talents inyofanya kazi ya kutafuta ,kuibua na kuendeleza vipaji katika michezo na sanaa,katika mpango huu pia tutajaribu kuvitangaza vipaji husika ili umma wa wa Tanzania na dunia kiujumla waweze kuwatambua watu hawa na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao.
Leo hii naomba nilete kwenue Nyota Mdogo kabisa wa kike anayefanya michezo ya mbinu za kujihami ya TAEKWANDO,nimeambatanisha maelezo yake pamoja na baadhi ya picha zake ili tuweze kumtangaza kwenye jamii kupitia vyombo vyetu hivi muhimu.
Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia:Kike
Miaka:12
Utaifa:TANZANIA
Mchezo: Taekwando
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
Makazi: Leuven Belgium
MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA & DHAHABU
Kijana wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde Brussels Belgium tarehe 27 May 2012.
Sasa hivi anajiandaa na team yake kwenda Copenhagen kwenye mashindano ya Wonderfull Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao.
Wito wake hasa kwa vijana wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA.
VIPAJI HUINUA TAIFA
AikaRose Mwasha akiwa na Mwanamichezo mwenzake baada ya shindano na kupata medali zao.
Copyrights Tabitha Hudson 2012
0 comments:
Post a Comment