Ads 468x60px

Saturday, August 11, 2012

Ajali Nyingine Morogoro...! Ni basi la Sumry


 basi la Shabiby lililokuwa likitokea
mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha
njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro
ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro
 Basi
la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es
Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea
ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea
mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha
njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro
ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro
Askari wa Kikosi cha Usalam Barabarani Wakiwa Eneo la Tukio
Mmoja
wa majeruhi wa ajali ya basi la Shabiby, Deogratias Mrai akiwa katika
wodi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro akiuguza
majeraha aliyopata kufuatia basi hilo walilokuwa wakisafiria kuacha
njia na kupinduka katika eneo la Mkundi-Makunganya Manispaa ya Morogoro
lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi
matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu
Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40
walijeruhiwa.
--
Na : Juma Mtanda

Kutoka
Morogoro -- WATU 45 wamejeruhiwa kwenye ajali baada ya mabasi matatu
waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka eneo la Mkundi kwa
Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, katika Barabara ya
Morogoro - Dodoma.



Ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi kwa kuhusisha mabasi matatu,
Kampuni ya Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam,
Allys Sport na Sumry yaliyokuwa yakitokea Morogoro kwenda Mwanza.



Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema
basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.



Mmoja wa abiria hao, Rashid Shaaban alisema baada ya basi hilo
kupinduka, ghafla waliona basi jingine la Sumry likiacha njia na
kupinduka wakati lilipojaribu kulipita gari jingine jirani na eneo
hilo.



Alisema kuwa wakati kukiwa na msongamano wa magari katika eneo hilo la
ajali, basi jingine la Allys Sport liliacha njia na kupinduka na hivyo
kutokea ajali tatu katika muda usiozidi dakika 10.



Shaaban alisema baada ya ajali hizo walitokea watu waliokuwa
wakijifanya kutaka kutoa msaada, lakini lengo lao lilikuwa ni kuiba
mali za majeruhi. Hata hivyo, alisema lengo lao hilo halikufanikiwa
kwani muda mfupi baada ya kutokea, askari walifika na kuimarisha
ulinzi.



Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari na wauguzi walionekana
kuzidiwa na wagonjwa kutokana na idadi kubwa ya majeruhi waliokuwa
wakihitaji huduma.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha
kutokea kwa ajali hizo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa
zimetokana na utelezi na mwendo kasi.

Copyrights Tabitha Hudson 2012

0 comments: