Ads 468x60px

Saturday, August 11, 2012

SERIKALI YAAGIZA SUKARI KUTOKA NJE ILI KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI



SERIKALI imeagiza
sukari Tani 29,1900 kutoka nje ya nchi
lengo likiwa ni  kushusha
mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali nchini kwa asilimia 17.4.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Baraza
Jipya la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, Waziri wa sekta hiyo, Dk William
Mgimwa alitabanaisha kwamba kutokana na utafiti uliofanywa na serikali kwa
mwezi Julai  umebaini ongezeko
la  asilimia 24.7  la bidhaa mbalimbali.
Alisema baadhi
ya  bidhaa kama Sukari, Unga, na
Mchele, zimeonekana zikipanda bei kwa kasi jambo ambalo linaashiria kuwaumiza
walaji sambamba na kudumaza uchumi wa nchi.
“Vyakula vipo
nchini, ila tatizo kubwa ni miundombinu kutokana na baadhi ya maeneo kuwa
chakavu na kusababisha mazao kushindwa kufika sokoni kwa wakati au kufika kwa
gharama kubwa” aliongeza Dk. Mgimwa.
Sambamba na hilo
serikali imetenga dola  sh milioni
600 sawa na shilingi bilioni 93 kwa ajili ya mradi wa kuzalisha gesi,
itakayosaidia usindikaji wa  bidhaa
viwandani sambamba na ajira.
Alifafanua kuwa
gesi hiyo itakuwa na uwezo wa kuzalisha megabaitsi 2000  jijini Dar es Salaam, na kusambazwa
katika viwanda, Kampuni, Taasisi pamoja na  sekta muhimu mbalimbali zinazozalisha uchumi wa nchi.

0 comments: