Mfuko
wa akiba ya wafanyakazi serikalini-GEPF- imesaini Mkataba wa kukopesha shilingi
milioni 200 kwa chama cha kuweka na kukopa –SACCOS- ya Bugando Medical Center
–BMC- kwa lengo la kuwanufaisha wanachama kwa mikopo yenye riba nafuu.
Akizungumza katika
hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya fedha hizo Mkurugenzi
Mkuu wa GEPF DAUDI MSANGI amesema mkopo huo ni mwanzo wa upopeshaji wa vyama
vya kuweka na kukopa nchini SACCOS hivyo wataendelea kuzikopesha saccos lakini
ni baada ya kuridhishwa na sifa za usalama wa fedha zao.
Amesema utoaji huo wa
mkopo kwa SACCOS ni hatua nyingine ya kujipanua zaidi ilikuwafikia kila
wanachama waweze kunufaika na mfuko wao wa akiba ambao una skimu mbili za
uchangiaji kwa lazima na uchangiaji wa hiari na ni kwa muda wa miaka 2 ambapo
marejesho yake yatatokana na kukatwa katika mishahara kwa wanachama hadi
kukamilika kwa deni hilo.
Naye Mwenyekiti wa
chama cha kuweka na kukopa –SACCOS- ya Bugando Medical Center –BMC- CLEMENT
KISHOSHA amesema mkopo huo wa shilingi milioni 200 unatarajia kunufaisha
wanachama 50 kati ya wanachama 700 ambapo kila mkopaji atakopeshwa kulingana
kiasi cha mshahara wake.
0 comments:
Post a Comment