MAAMBUKIZI
ya Ugonjwa wa Ukimwi Wilayani Gairo Mkoani Morogoro yamepungua kutoka asilimia
3.2 mwaka 2011 mpaka asilimia 2.7 mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Severin Lalika kwenye mafunzo ya kuyajengea uwezo
mabaraza ya kudhibiti maambukizi ya VVU-Ukimwi wilayani humo yaliyoaandaliwa na
tume ya kudhibiti maambukizi hayo (TACAIDS)kutoka wilayani Kilosa .
Warsha hiyo
iliyowashirikisha wajumbe wa kamati hiyo toka kata nne,taasisi na asasi
mbalimbali zikiwemo za dini na kijamii zinazopambambana na maambukizi hayo
wilayani humo inakusudi kuweka mikakati ya kuzikabili changamoto za maambukizi
wilayani humo.
Lalika alisema elimu na
mafunzo kutoka kwa wataalam mbalimbali ndio sababu kubwa ya mafanikio hayo huku
akiwataka wajumbe hao kuzingatia mafunzo hayo ili yawe na tija kwa jamii
wakizingatia kuwa ni fedha za wanachi zinazotumika katika mapambano.
Awali Mratibu wa Ukimwi
Wilayani Kilosa Delfina Pacho aliwataka wajumbe hao kuzingatia mafunzo kwani
yanaumuhimu mkubwa kwa jamii katika kupambana na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment