Ads 468x60px

Saturday, July 13, 2013

Saudia yawaonya mahujaji kuhusi hatariu kirusi hatari

                                                                 
Wizara ya Afya nchini Saudi Arabia imetoa onyo kwa Mahujaji na kuwataka wavae (mask) katika maeneo yenye misongamano mikubwa ili kuzuia kuenea kirusi hatari.( Kirusi hicho kinashabihiana na kile cha SARS ambacho kiliua karibu watu 800 mwaka 2003.)

Katika taarifa yake Wizara ya Afya Saudi Arabia imetoa orodha ya masharti kwa mahujaji wanaopanga kutembelea maeneo matakatifu nchini humo ili kuzuia kirusi kijulikanacho kama Middle East Respiratory Syndrome coronavirus (MERS-CoV). Taarifa hiyo imewataka wazee na wale wenye magonjwa sugu kuakhirisha safari za Hijja au Umra.

Hadi sasa watu 38 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia kutokana na kirusi hicho hatari. Maafisa wa afya wa Saudi wamewataka watu wote wadumishe usafi binafsi katika maeneo ya umma, watumie kikaratasi au kitambaa wanapopiga chafya au kukohoa na wawe na chanjo zote zinazohitajika.

Msimu wa Hija mwaka huu utaangukia Mwezi Oktoba, pamoja na hayo Waislamu hufanya ziara katika miji mitakatifu ya Makka na Madina katika kipindi chote cha mwaka. Kirusi cha MERS-CoV kiliibuka mara ya kwanza nchini Saudi Arabia Septemba mwaka 2012 na kimesharipotiwa Jordan, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Tunisia na Uingereza.

0 comments: