Ads 468x60px

Thursday, August 23, 2012

BENDI YA MSONDO NGOMA YATANGAZA RATIBA YA WIKI





BENDI
kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’
imetoa ratiba yao katika wiki baada ya mpambano wao mkali na mahasimu
wao Sikinde uliofanyika Jijini Dar es salaam pamoja na Zanzibar baada ya
kutoa burudani ya Iddi sasa wamerudi kwa ajiri ya kutoa burudani 
ambapo wamesema
kuwa wataanza kutoa burudani siku
ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosiwatakuwa  Kilimani Pub Staki Shari, na jumapili watamariza wiki endi katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni











Akiongea
, Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua
kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea baada ya kusherekea sikukuu .










“Msondo
ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba,
hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetu kwani bila
wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema Super D.






Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa
Sabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo
Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba
zamani zikiwemo Asha Mwanasefu,Cheusi Mangara,mwana Mkiwa na nyingine
nyingi zilizotamba kipindi hicho

0 comments: