Ads 468x60px

Thursday, August 23, 2012

TASWIRA ZA MABOMU YA MACHOZI YALIVYORINDIMA MTAA WA KONGO KARIAKOO JANA MARA BAADA YA VURUGU KUZUKA









Mmoja wa majeruhi wa mabomu ya machozi kwenye vurugu hizo akiondolewa
eneo la soko la Kariakoo baada ya kuanguka chini kutokana na milipuko
hiyo, ambayo iliambatana na mawe yalikuwa yakirushwa na vijana waliokua
wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Askari wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia FFU wakiweka ulinzi
mkali eneo la Kariakoo baada ya kufunga mtaa wa Kongo na ya jirani
kutokana na kuibuka vurugu zilizotokana na ugomvi wa nyumba ambayo kwa
maelezo ya watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya
miaka 20 kati ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati
feki.
Mitaa ya Kituo cha Polisi Msimbazi Kariakoo ikiwa mitupu bila ya watu
wengi kama ilivyozoeleka ni askari tu ndio waliokuwa wakiranda kwenye
eneo hilo.
Mtu
ambaye alijitambulisha kuwa ndie mwenye nyumba hiyo ambayo inamilikiwa na
mama yake, ambapo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameipigania
haki yao kwa miaka ishirini hadi leo wanaipata kutokana na kesi
waliyofungua mahakamani wakidai kunyang'anywa nyumba yao na wapangaji
kwa kutengeneza hati feki.
Nyumba inayo gombaniwa na kuzua tafrani kabla haijaanza kuvunjwa eneo la mtaa wa Kongo Kariakoo.




Hapa vijana wa kazi wa kampuni ya Yono Auction Mart iliyopewa tenda
ya kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo chini ya ulinzi mkali wa pilisi
wakiendelea na kazi kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Kongo


Mashuhuda nao walikuwepo tangu zoezi linaanza na walikuwepo pia
wanaoufahamu mgogoro huo na kudai kuwa nyumba hiyo anadhulumiwa mzaramo
na Mwarabu kwasababu anapesa, lakini wengine wakasema nyumba hiyo
imeuzwa mara tatu tofauti na kuzua mgogoro huo.
 Mtaa wa Kongo ukiwa hauna mweupe
 Mtaa wa Mchikichini Kariakoo ukiwa hauna watu kutokana na vurugu zilizotokea jana
 Mtaa wa Mkunguni ambao huwa na pilikapilika nyingi ukiwa mtupu kufuatia wafanyabiashara kufunga biashara zao



 Askari
Polisi wakimdhibiti mmoja wa vijana waliokamatwa katika vurugu
zilizotokea katika mtaa wa Kongo na Mchikichi jijini Dar es Salaam jana
kufuatia mgogoro wa kugombea nyumba namba 86 inayomilikiwa na Samiri
Said
 Askari Polisi akiweka mabomu ya machozi katika bunduki yake huku akiangalia hali ya usalama wake.
 Askari Polisi akijiandaa kurusha mabomu ya machozi ili kukabiliana na vijana waliokuwa wakirusha mawe.Picha Zote na Francis Dande wa HABARI MSETO BLOG

DAR ES SALAM, Tanzania

RISASI
na mabomu ya kutoa machozi jana vilirindima katika maeneo ya Kariakoo
baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni
yake.

Hali
hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda
kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu
huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba
hiyo.

Akizungumza
katika eneo la tukio kiongozi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Isaac
Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya Mahakama kwa lengo la
kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.

Amesema
kuwa hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi
walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan
kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.

Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.

“Vijana
hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoka kila
kona walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua
risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya mbali”
alisema Nguku.

Baada
ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguka nyumba hiyo
ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na
Mchikichini

Naye
mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika
nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati
bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.

Alisema
kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako
waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi
huyo  kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.

Nyumba
hiyo inayogombewa iko mtaa wa Karikoo kitalu namba 86, hata hivyo
wakati zoezi hilo likiendelea mvamizi huyo alikuwa  ndani kwa ajili ya
kutumikia kifungo cha siku 21.




Copyrights Tabitha Hudson 2012

0 comments: