Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri, ameagiza kukamatwa kwa kiongozi mkuu wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie ambapo analaumiwa kwa kuchochea ghasia zilizotokea mjini Cairo ambapo watu 51 waliuawa.
Amri ya kuwakamata viongozi wengine wapatao 100 wa kundi la Brotherhood imetolewa na baadhi wamewekwa kizuizini ambapa agizo hilo linajiri wakati Waziri Mkuu mteule yuko mbioni kuteua serikali mpya baada ya kuondolewa madarakani kwa Mohammed Morsi.
Chama cha kisiasa cha Freedom and Justice Party kimesema hakitajiunga na utawala wa mpito na kimekataa wadhifa wa uwaziri kilichotengewa na Waziri MKuu Hazem al-Beblawi.
Msemaji wa Muslim Brotherhood Gehad El- Haddad ameambia vyombo vya habari kwamba amri ya kumkamata Badie ni njama za jeshi kuzima maandamano na kulaumu jeshi kwa kuwafyatulia risasi waandamanaji wakati wakifanya maombi nje ya kambi kuu ya jeshi.
0 comments:
Post a Comment