Ads 468x60px

Wednesday, July 10, 2013

MARANGU




MARANGU
KUFUATIA tukio la moto lililotokea katika hifadhi ya msitu wa mlima Kilimanjaro Julai saba mwaka huu kushika kasi katika maeneo ya Rombo na Kilema, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas  Gama ameziagiza Wilaya zote za mkoa huo, kutoa askari mgambo  walioko katika wilaya zao  kushiriki operesheni maalum  ya kuzima moto huo.
Tayari watu zaidi ya 200 wakiwemo  askari walioko kwenye mafunzo katika Chuo Cha Polisi Moshi wameendelea kushirikiana kuuzima moto huo ambao mpaka sasa wamefanikiwa kudhibitii moto huo  kwa asilimia 75.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea neo hilo Meneja mahusiano kutoka hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete  alisema moto huo ulioanza siku ya jumapili julai saba umeendelea kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa bila kuathiri shughuli zozote za utalii katika hifadhi ya mlima.

Alisema moto huo ambao sasa unawaka  katika maeneo mawili tofauti ikiwemo eneo la Rombo  na  Kilema juu  imewalazimu kuweka kambi mbili tofauti  ambapo kambi ya moja imewekwa  eneo la Marangu  kwa wanaozima msitu uliopo Kilema juu  huku kambi nyingine ikiwa imewekwa Rombo kwa wale wanaozima maeneo ya Rombo.

Alisema moto huo umeathiri zaidi maeneo ya Amboni,Ushiri,Keryo,Kimori na Shimbi na kwamba kwa sasa jitihada zinafanyika kuhakikisha moto huo unakwisha  na kwamba mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha moto huo ni watu waliokua wakirina asali kiholela waliwasha moto katikati ya m situ.

Alisema licha ya moto huo kuwa mkubwa na kuunguza zaidi ya hekari 40 haujaathiri shughuli zozote za kitalii zinazoendelea katika hifadhi ya mlima huo na kwamba shughuli zote za kitalii zinaendelea kama kawaida.

Alisema hifadhi ya Taifa kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaendelea na juhudi za kutafuta waliohusika na uharibifu huo na mara zoezi  la kuuzima moto litakapokamilika taarifa ya tathmini ya madhara ya moto itafanywa.

Hii ni mara ya pili moto mkubwa kuwaka katika eneo hilo hilo ambapo moto kama huo uliwaka mwaka 2009 na kusababisha hasara kubwa  kwa misitu na viumbe hai.

0 comments: