Halmashauri ya Wilaya
ya Babati vijijini, Mkoani Manyara imefuta rasmi leseni zote za biashara
zilizokatwa kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 kabla ya muda halisi wa mwisho wa
kutumika kwa leseni hizo mwezi julai mwaka huu.
Kwa mujibu wa agizo
hilo lililotolewa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Babati vijijini Dominic Kweka
katika kata ya Bashnet, leseni zote za biashara zilizoishia juni 30 mwaka
huuzinatakiwa zikatwe upya kwa ajili ya matumizi ya kuendeshea biashara husika.
Kweka amesema kuwa kila
mfanyabiashara anatakiwa kukata upya leseni yake na mwisho wa zoezi hilo ni
julai 8 mwaka huu na kuanzia Julai 9 wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo
watakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha ameeleza kwamba
uamuzi huo umetokana na mabadiliko ya bajeti ya Serikali kwani awali ilikuwa
ikisomwa kila mwezi juni na mwaka huu imekuwa tofauti ambapo ilisomwa mwezi
April, hivyo kubadili mfumo wa ubadilishwaji wa leseni hizo.
Hata hivyo baadhi ya
wafanyabiashara katika kata hiyo wamedai kwamba Serikali haikuwatendea haki
kwani kabla ya kutoa matangazo hayo ingekaa na nao na kuwaelimisha juu ya jambo
hilo.
0 comments:
Post a Comment